Burudani

Fid Q afikiria kuwapeleka kortini Orijino Komedi kwa kumchafua, lakini…………

Baada ya Orijino Komedi kumshutumu rapper Fareed Kubanda aka Fid Q kuwa amecopy na kupaste beat ya wimbo wake Danger, rapper huyo hajaridhika na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kiasi cha kufikiria kutafuta mwanasheria ili awaburuze kortini waigizaji hao.

“Looking for a good lawyer dealing with defamation of character cases.. Contact us for details,” Fid alitweet jana.

Baada ya kuona tweet hiyo, Bongo5 ilimpigia simu rapper huyo kutaka kujua kama kweli amedhamiria kulipeleka suala hilo kwenye sheria na yeye kusema kuna watu walimshauri afanye hivyo lakini ameamua kupuuzia.

Hata hivyo alisema suala hilo limemuumiza kwakuwa watu wasiofahamu masuala hayo wamemchukulia tofauti.

“And you know one of the things that I hate nowdays is taking everything for granted. Unajua kilichoniuma ni kwamba ingekuwa Ulaya, watu Ulaya wanajua lakini sasa Bongo unapowaambia hivyo watu wanaamini hundred percent,” alisema.

Aliongeza kuwa amekuwa akipata ujumbe kupitia Facebook unaomkera kwakuwa watu wamepotoshwa na Orijino Komedi.

Staa huyo wa ‘Sihitaji Marafiki, aliiambia Bongo5 kuwa atahitaji Orijino Komedi wamemuombe radhi rasmi kwa kuchafua jina lake.

Wiki hii studio iliyotengeneza beat hiyo iliamua kutoa tamko na kuwashutumu Orijino Komedi kwa kukurupuka kuongea kitu wasichokifahamu.

“Chofaco Records owns full copyright of the song Danger by Fid Q, produced by chobaray.Nyimbo ilirekodiwa November,2008,jiulizee nyimbo ilitoka mwaka gani?mziki wa USA sio sawa na mziki wa Bongo. Kuna tofauti kati ya mixtape songs and album songs also released tracks,non exclusive tracks and exclusive tracks,kabla orijino komedi kukurupuka na kuongea/kufanya vipindi vyao lazima mjue copyrights za kazi za watu,heshima na busara,kuuliza na kuelimishwa si ujinga.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents