Burudani

Fid Q afunguka ishu ya Ben Pol na picha za ‘utupu’

By  | 

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop Fid Q ambaye anadaiwa kuwa mshauri mkuu wa Ben Pol katika shughuli za muziki amefunguka kuzungumzia ishu ya muimbaji huyo kupiga picha za utupu na kusambaza mtandaoni.

Fid Q

Mapema leo mkali huyo wa wimbo ‘Phone’, kupitia mtandao wa Instagram alipost picha zikimuonyesha sehemu zake za mwili ambazo hazipaswi kuonekana wazi.

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha U-Heard cha Clouds FM, Fid Q amedai hajashauriana na Ben Pol kuhusu picha hizo zinazosambaa mtandaoni na hajui chochote kinachoendelea.

“Sijajua anataka kuongelea nini kwenye ile cover na mimi nasubiria kuangalia nini kitatokea, siwezi kusema ni kitu kibaya au kizuri kwa sababu sijajua nini anataka kufanya” alisema Fid Q.

Aliongeza, “Kwahiyo hata mimi sijui ana maana gani ndio maana nikasema tusubirie tuona ana kitu gani anakuja nacho ndipo tuanze kuzungumza kwamba ni ishu mbaya au nzuri,”

Pia rapa huyo amewataka wasanii kufuata maadili ya kazi zao kwa kuwa wasanii wakongwe waliweza kufanya muziki mzuri na kuwashawishi wazee kuamini muziki sio uhuni.

“Nijaribu kuwakumbusha wasanii kwamba muziki sio uhuni, tumeweza kuwashawishi wazee wetu kuamini muziki wetu sio uhuni ndiyo maana mpaka leo umeweza kufika hapa. Kwahiyo mimi ningesema wasanii wanatakiwa kufanya kazi nzuri ambazo zitaweza kuwafanya wao kufanya vizuri zaidi,”

Wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamepinga tukio hilo huku wakidai muimbaji huyo sio msanii na matukio hayo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments