Burudani

Fid Q aipinga hatua ya serikali kuuita uwanja wa ndege wa Mwanza ‘Serengeti International Airport’

Hivi karibuni serikali imeridhia kubadilishwa kwa jina la uwanja wa ndege wa mkoa wa Mwanza utakapokamilika na kuitwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Serengeti.

Mabadiliko hayo ya jina la uwanja wa ndege ni sehemu ya utangazaji na mkakati wa kukuza utalii kwenye mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ni rahisi watalii kufika katika mbuga ya wanyama ya Sengereti wakitokea Mwanza.

Hata hivyo watu wengi hasa wenye asili ya Mwanza hawajafurahishwa na uamuzi huo akiwemo rapper Fareed Kubanda aka Fid Q ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

Kupitia Twitter, jana ameandika, “Kiukweli kuna watu wanajua sana kunikera. Mnataka kuniambia huyo mbunifu wa jina jipya la airport ya Mwanza Serengeti Airport aliumiza kichwa?”

“Imagine: Mbeya pajengwe airport halafu iitwe Mikumi Airport au Tanga halafu iitwe Mwadui Airport au Dar halafu iitwe NyamaganaAirport???”

Mjadala huo ulivutia hisia ya watu wengi akiwemo mtangazaji wa Clouds FM aliyehoji, “ Why do we have Nyerere Aiport in Dar while he is from Musoma? Au alikua raisi wa Dar?”Fid alijibu, “Zaidi ya Rais,yule ni ‘BABA WA TAIFA.”

“Kuna mambo mengi ya kutilia maanani kabla ya kutoa jina eg maana, historia, way foward/madhara/ etc warudi kwa wadau,” alitweet mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji.

Kwa upande wake mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye alihusika katika kupendekeza jina hilo alisema, “Anyway let mwanza people decide. May be it was wrong for us to suggest that. However I think Serengeti International Airport is okay. Tanzania is branded as The Land of Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar. Serengeti belongs to Tanzania, yote sio Mara tu.”

Mfano huo wa Zitto ulipingwa kwa swali na Fid aliyehoji, “Je mtaenda kujenga airport Kigoma halafu muiite Ngome Kongwe Airport kwasababu ni brand name pia???”

Fid alipendekeza majina ambayo yangepaswa kutumika kuuita uwanja huo kwa kutweet, “Sangara International Airport…..Nyanza International Airport…..now loading names of Mwanza heroes. Mfano wa vivutio, Bismarck rock, Saa Nane island, Kijereshi etc.”

“The biggest damage school does to us is learning that “WE CANT BELIEVE OUR OWN EXPERIENCE”*sasa tunaipindisha history kwa ajili ya touri$m?” alihoji tena Fid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents