DStv Inogilee!

Fid Q alilia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar


Wakati watanzania wakiwa kwenye mjadala mzito kufuatia maandamano ya juzi visiwani Zanzibar ya kuupinga muungano, rapper Fid Q amesema kuvunjika kwa Muungano ni mwanzo wa Tanzania kuyumba.

“Muungano- united we stand, divided we fall!!” alitweet.

Fid amesema wazanzibar wana haki ya kudai matakwa yao juu ya muungano lakini si kwa kufavya vurugu, “ndo maana nikasema.. Mie binafsi nina amini ile sio njia sahihi ya kufikishia ujumbe.”

Katika hatua nyingine Fid ambaye jina lake halisi ni Fareed Kubanda amesema kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kuandika vitabu pamoja na kuzifanyia kazi documentaries kadhaa.

Katika utaratibu wa kila weekend aliyojiwekea msanii huyo kujibu maswali ya mashabiki wake, Ngosha amejibu swali la kama anakumbuka show yake ya kwanza ilikuwa wapi na alilipwa kiasi gani ambapo alijibu, “Mwanza.. Nililipa mlangoni!!’

Jibu hilo linatukumbusha filamu ya Girlfriend iliyoigizwa na Crazy GK, TID, Jimmy Kabwe, Monalisa na wengine ambayo ilionesha jinsi wasanii walivyokuwa wakiwambembeleza madj ili wapewe nafasi ya kuperform.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW