Burudani

Fid Q atoa Darasa kwa ma-director wa video Bongo

Msanii wa hip hop Bongo, Fid Q amewapa somo madirector wa video kutoka Bongo kwa kuwataka kutoamini katika kufanya kazi pekee yao.

Rapper huyo amesema kipindi cha nyuma madirector walikuwa wakilalamika kuwa wasanii hawawapi bajeti ya kutosha na ndio sababu ya kufanya video chini ya kiwango lakini hata pale walipopewa bado hakuna kilichobadilika.

“Kwa hiyo shida ikawa siyo bajeti suala ni namna wanavyofanya wao masuala ya quality ya picha na color grade. Sasa hivi madirector wa Bongo wapo vizuri na kama haitoshi siku hizi wamekuwa na DOP (director of photo) ambao wanachukua picha nzuri, kwa hiyo tumeanza kupata video kama za South Africa na sisi,” ameiambia Ladha 3600 ya E Fm.

“Wanasema give credit panapo husika, kwa hiyo naomba niwape pongezi hizo wanafanya kazi nzuri, cha msingi wasiamini katika kufanya kazi wao pekee yao bila hata kushirikiana,” amesema Fid Q.

Ameongeza kuwa “unajua kuna siri moja ya ndani kidogo watu hawajui, unajua GodFather hafanyi mwenyewe zile video yeye anadirect tu halafu anachagua nani ataenda kuedit, GodFather sio mnyama wa video yeye anajua nani afanye naye kazi”.

Fid Q kwa sasa anafanya vizuri na ngoma zake mbili mpya ambazo ni Fresh na Ulimi Mbili.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents