Burudani

Fid Q kufanya listening party ya album yake ‘Kitaaolojia’ Alhamis hii Nairobi, album itatoka July

Fareed Kubanda aka Fid Q Alhamis hii atafanya listening party ya album yake mpya, Kitaaolojia jijini Nairobi, Kenya.

UC 2013 FB COVER 2
UC 2013 FB COVER 2

Party hiyo itafanyika kupitia mradi wa Nairobi Rapsody kwenye kiota cha Ebony Lounge jijini humo.

Album hiyo itaingia sokoni mwezi ujao na itakuwa na nyimbo 10 zikiwemo Ielewe Mitaa, Neno aliyofanya na Lord Eyez, Sihitaji Marafiki aliyomshirikisha Yvonne Mwale kutoka Zambia, Siri ya Mchezo aliyomshirikisha Juma Nature, Bendera ya Chuma akiwa na Ben Pol na Bongo Hip Hop aliyomshirikisha P Funk Majani.

Pia kwenye album hiyo kutakuwepo na wimbo ambao Fid amewashirikisha Sauti Sol. Fid pia ni miongoni mwa wasanii waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio Africa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents