Burudani

Fid Q na Bonta wazungumza waliyojifunza kwenye uchaguzi wa Marekani


Kuanzia asubuhi ya leo, mada iliyotawala vichwa vya wengi ni ushindi wa Barack Obama ambaye ameingia ikulu kwa awamu ya pili baada ya kumshinda mpinzani wake Mitt Romney kwenye uchaguzi wa jana.

Tumezungumza na wasanii wawili wa Hip Hop nchini ambao wamekuwa wafuatiliaji wazuri wa siasa za kimataifa, Fareed Kubanda aka Fid Q na Bonta aka Maarifa.

“Watanzania ambacho wanapaswa kujifunza ni ule mchakato mzima wa jinsi uchaguzi unavyoendeshwa kila kitu kilivyokuwa wazi japokuwa nimeona baadhi ya watu wakilalamika kwamba kuna sehemu ambazo Mitt Romney alitaka afanye uchakachuaji hasa sehemu anayotokea,” anasema Fid.

“Kwahiyo uchakachuaji upo sehemu zote lakini inategemea na ilivyo. Kwahiyo uchaguzi ulikuwa ni wa haki na unaonesha kabisa kuwa kila kitu kinahesabiwa na mtu anakabidhiwa hapo hapo na nimependa zaidi mpinzani anapokuwa anahusishwa katika kukubali matokeo. Safari hii ukiuchunguza vizuri huo uchaguzi kulikuwa na setbacks nyingi sana kwa Obama especially kwakuwa Mitt alikuwa ana support ya corporate wengi kwahiyo hiyo corporate money unajua how powerful it is, jamaa ameweza kupita kwasababu jamaa tu ni kichwa yaani.

Uchaguzi wa kule unaweza ukaupredict hata katikam debate zile walizokuwa wanafanya, aliposhindwa mara ya kwanza Obama, dunia nzima ilitingishika kwamba jamaa kashindwa. Halafu kitu kingine kuna mtu ametweet amesema kwamba “Obama amesababisha wahuni, wavuta bangi, akinadada wanaojiuza watu wote wanaofanya mambo ya ajabu ajabu kufuatilia uchaguzi ni nani mwingine ambaye ana uwezo huo duniani? Kwahiyo kuna vitu unatakuwa kuviangalia kwamba huyu mtu yuko powerful na amebarikiwa. Hoja ya msingi ambayo nimeipenda, Obama ameshinda lakini bendera inayopepea hapo nyuma sio bendera ya chama chake ni bendera ya nchi hiyo ndio true definition ya mtu anaposema kwamba anafanya hii kitu kwasababu ya watu.

Kwa upande wake Bonta amesema, “Kitu ambacho mimi nimekiona ni kwamba kuna hali ya uwazi ilikuwa ni kubwa zaidi, tunasema ile sasa ndio democracy sababu unajua democracy ina pillar zake tatu na zile pillar tatu za democracy ya kwanza zaidi ni transparency. Sasa kama uliona uchaguzi wa Marekani kuanzia jana mida ya moja moja ukiingia kwenye vyombo vya habari unaona ile graph ilivyokuwa inaenda kulikuwa na uwazi kila kitu kilikuwa transparent na kila mtu alikuwa anajua trend inaenda vipi mpaka mwisho imekuja kuonekana Obama ameshinda.

Bonta pia amezungumzia kuhusiana na vyombo vya habari kuepukana na mtindo wa kushabikia watu pamoja na propaganda hususan za kuchafua majina ya watu ama kuwapandisha baadhi ya wanasiasa.

Pia amesema ushindi wa Obama hautakuwa na faida kubwa kwa waafrika kwakuwa anaongoza nchi hiyo kwa kufuata sera za nchi yake ambazo si tu kusaidia nchi za Afrika.

“Sisi tunashabikia kwasababu Obama ni mweusi unaujua. Waafrika wengi, watanzania, wakenya wengi tumekuwa wabaguzi. Watu wengi tunamshabikia Obama kwasabababu ni mtu mweusi sasa hiyo ndio tunasema ‘apartheid policy’ kwahiyo hata wazungu wakilalamika watu wa Tanzania wa Kenya wamekuwa wabaguzi hatuwezi kukataa.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents