BurudaniEventsHabari

Fiesta 2007 Yaja Tena

Kevin LyttleMara ya mwisho tamasha hili la Fiesta lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club maeneo ya kinondoni ambapo maelfu ya watu walimiminika kwa shangwe ukizingatia wahusika na waandaaji wa tamasha hilo walitangaza kuwa ni la mwisho lakini safari hii wamekuja kwa staili mpya wakidai ni FIESTA SHANGWE BODA KWA BODA.

Kevin Lyttle

 

Mara ya mwisho tamasha hili la Fiesta lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club maeneo ya kinondoni ambapo maelfu ya watu walimiminika kwa shangwe ukizingatia wahusika na waandaaji wa tamasha hilo walitangaza kuwa ni la mwisho lakini safari hii wamekuja kwa staili mpya wakidai ni FIESTA SHANGWE BODA KWA BODA.

 

Unaweza kuona ubunifu ambao umefanyika katika kulirudisha tamasha hili, waandaaji wameamua kulipenyeza tamasha hili mpaka katika boda za Kenya na Uganda, ambapo safari hii inaonesha ukomavu katika utanuaji wa mipaka na kuitangaza sanaa ya watanzania.

 

Fiesta 2007 inatarajiwa kuanzia maonesho yake katika mji wa Mwanza na kufuatiwa na Bongo D’salaam ambapo mikoa mingine kibao itafuatia.

 

Kama ilivyo kawaida ya Tamasha hili hukutanisha wasanii kutoka sehemu mbali mbali ambapo mwaka jana msanii Ja Rule aliweza kujimix na wabongo na kupiga bonge ya show, je safari hii nani atashuka? Haya ni maswali ambayo watanzania na wapenzi wa burudani kwa ujumla wamekuwa wakijiuliza.

 

Safari hii Ili kuifanya Fiesta iwe na mtazamo wa kiafrika zaidi anatarajiwa kushuka msanii Koffie kutoka Congo, Kevin Lyttle kutoka Jamaica, Ngoni toka Uganda, Mr Lenny wa Kenya na wasanii wnegine kibao.

 

Wasanii kama Joh Makini, TMK Wanaume, Wanaume Halisi, Chidi Benz, Jay Moe na wengine kibao wanatarajiwa kupanda katika jukwaa la Fiesta 2007.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents