Michezo

FIFA kutoa beji 18 kwa waamuzi wa Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), limetoa beji 18 kwa waamuzi wa Tanzania msimu wa mshindano mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni Mfaume Ali, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina Zablon.

Mwamuzi wa kike wa Kimataifa wa Tanzania,  Jonesia Rukyaa ambaye ni miongoni mwa watakao pata beji hiyo ya FIFA

Waamuzi Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli, Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na kwa wanawake Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace Wamala.

Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents