Michezo

FIFA Kuzibana Timu Kusajili

 

Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA) litatumia njia ya mtandao kuongoza uhamisho wa kimataifa wa wachezaji wa mpira ilii kuondoa matumizi ya fedha haramu na rushwa kwenye soko la soka.

‘Huu ni wakati wa kihistoria kwenye soka’ alisema Rais wa FIFA, Sepp Blatter.

Mfumo huo mpya unatarajiwa kutumika na klabu za soka 3,500 kutoka kwenye nchi zaidi ya 150. Lengo kubwa la mfumo huo ni kuondoa matatizo ya baadhi ya mawakala kuwamiliki wachezaji wao, malipo yasiyo halali kati ya klabu na kampuni,na usafishaji wa fedha haramu kupitia uhamisho wa mchezaji.

Viongozi wa Fifa walikataa kuongelea lolote kuhusu jinsi gani wapelelezi watakuwa wanafuatilia uhamisho wa mchezaji lakini walisisitiza kwamba adhabu kali zinazisubiri klabu ambazo zitakazo vunja sheria hiyo ikiwa ni pamoja na kufungiwa kusajili wachezaji, kutozwa faini na kuporwa pointi.

‘Ukitumia mfumo wa kwenye mtandao huwezi kudanganya,’ alisema kiongozi wa sheria wa FIFA Marco Villiger. Kama mnunuzi wa muuzaji atatoa taarifa tofauti mchezaji hata hama timu. Mambo yote hayo yatakamilishwa kipindi cha usajili,na FIFA imetengeneza muda maalumu kwenye mtandao ili kuweza kuondoa matatizo yoyote ya usajili wa dakika za mwisho kama ilivyotokea kwa Andrei Arshavin alivyohamia Arsenal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents