Michezo

FIFA yaishutumu Afrika Kusini kwa kutoa hongo kuandaa Kombe la Dunia la mwaka 2010

Shirikisho la soka duniani FIFA limeishtumu Afrika Kusini kwa kulipa hongo ya dola milioni 10 ili kupewa fursa ya kuandaa kombe la dunia la mwaka 2010,kulingana na ripoti ya gazeti la Telegraph nchini Uingereza.

160316124531_afrika_kusini_2010

Fifa ilitoa ”taarifa ya mwathiriwa” na ”ombi la kurudisha fedha” hizo kwa afisi ya wakili wa Marekani,gazeti hilo limeongezea.

Maafisa wa Afrika Kusini wamesisitiza kuwa hawakulipa hongo.

FIFA inajaribu kukomboa makumi ya mamilioni ya fedha zilizochukuliwa kinyume cha sheria na wanachama wa shirikisho hilo pamoja na mashirika mengine ya soka.

Maafisa wa zamani wa shirikisho hilo Chuck Blazer na Jack Warner pamoja na Jeffery Webb ni miongoni mwa wale waliofunguliwa mashtaka na Fifa ambayo imewasilisha stakhabadhi kwa mamlaka ya Marekani.

FIFA imekuwa katika mgogoro tangu madai ya ufisadi kugunduliwa mnamo mwezi Mei 2015.

Kwa jumla watu 41 pamoja na kampuni kadhaa zimeshtakiwa na mamlaka ya Marekani.

Uchunguzi wa Marekani ulifichua ufisadi mkubwa katika shirikisho hilo na Fifa inakadiria kwamba mamilioni ya madola yaliibwa kupitia hongo,kiinua mgongo na mipango ya ufisadi iliofanywa na washtakiwa.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents