Michezo

FIFA yaipiga marufuku Nigeria kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa

Shirikisho la soka duniani (FIFA ) limeipiga marufuku Nigeria kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
nigeria
Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini.
Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.

FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.

Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.

FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.
Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15)

Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.

Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil.

Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn’goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents