Michezo

Fifa yatangaza viwango vipya vya timu za taifa

Shirikisho la soka duniani (FIFA) leo Agosti 11 limetangaza orodha mpya ya viwango vya kila mwezi kwa timu za mataifa yote duniani huku Argentina ikiendelea kuongoza kwenye chati hizo.

fifa

Timu ya Argentina inaendelea kushika namba moja kama timu bora zaidi duniani huku ikiwa na pointi 1585 ikifuatiwa na Ubelgiji (1401), Colombia (1331), Ujerumani (1319) na nafasi ya tano imechukuliwa na Chile yenye pointi 1316.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshuka kwa nafasi moja kutoka 123 mpaka nafasi ya 124 na imefanikiwa kupata pointi 300 ikishika nafasi ya tano kwa nchi za Afrika Mashariki ikiongozwa na Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Aidha viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika timu ya taifa ya Algeria ndiyo inaongoza ikiwa nafasi ya 32 huku ikiwa na pointi 781 ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne.

Bonyeza hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents