Bongo Movie

FIFII: Serikali ikitupa sapot tutafika mbali

Mwanamama Tumaini Bigilimana ni msanii wa maigizo ambaye kiutendaji ni tofauti na muonekano wake, jina la kisanii anaejulikana kama Fifii. Ni msanii wa muda mrefu aliyeanzia sanaa yake tangu alipokuwa mkoani kigoma ambako ndiko alipozaliwa na kukulia kisha kuhamia jijini Dar Es Salaam na kuendeleza sanaa yake.

Msanii huyo aliyeanza kuonekana katika tamthilia ya Ua jekundu na kuja kuibukia kwanye tamthilia ya Zeze ambayo ilikuwa ikirushwa kwenye televishen ya TVT ambayo kwa sasa ni TBC1.

 

Fifii amekuwa akipigana kufa na kupona kila kukicha katika kuendeleza sanaa ya Bongo na sasa ameibuka na hili “Serikali yetu imetutupa kabisa kwani ninaamini kama itawekeza huku kwenye sanaa ya maigizo ni lazima tufike mbali zaidi ya hapa tulipo”

Akiongelea kuhusu sanaa ya bongo Fifii alisema kuwa, sanaa ya bongo kwa sasa imepanuka na imekubalika katika sehemu kubwa ya bara la Africa na hata baadhi ya nchi za ulaya”  aliongeza kuwa “kutokana na kupanuka huko kwa sanaa yetu imefikia hata baadhi ya watu kujifunza Kiswahili ili kuweza kuelewa kile wanachokiangali”.

Kwa upande wa soko alisema kuwa soko bado ni gumu kutokana na wasambazaji kuwa wachache hivyo kufanya hata wasanii wachanga kushindwa kufanya vizuri kutokana na kazi zao kukaa muda mrefu zikisubiria foleni ya kuingia sokoni “soko bado ni gumu sana kwa kuwa wasambazaji ni wachache, na hao wachache wenyewe wanataka kusambaza kazi za wasanii wenye majina tu na kuwaacha wasanii wanaochipukia hivyo kuendelea kuwaona wasanii ni walewale tu kila siku lakini kiukweli wasnii wako wasio na majina likini wana kazi za ukweli kabisa hivyo serikali ikiingiza mkono wake katika kuongeza wasambazaji nadhani tutasonga mbele”.

Fifii ambaye kwa sasa ni anafanya kazi zake yeye mwenyewe akiwa kama producer na filamu yake ya kwanza ikiwa ni Kizungumkuti, huku matarajio yake ni kuja kuwa mtayarishaji wa kimataifa zaidi na kuipeleka sanaa ya bongo katika levo za kimataifa. Pia ana tarajia kuwa ni mmoja kati ya wasambazaji wa kazi za wasanii hapa nyumbani na hata Africa mashariki na kati.

Kwa upande wa challenge amesema hazimtishi wala haziogopi kwani anaamini bila challenge huwezi kufikia malengo.
Fifii pia aliiomba serikali kutuona kama sisi kamani waelimishaji hivyo watupe nafasi ya kutumia location za serikali kama vile mahakama uwanja wa ndege, vituo vya polisi na sehemu nyinginezo ilimradi watoe vibali maalum kwa ajili ya kutumia sehemu hizo.

Fifii amtoa ushauri kwa wasanii wengine katika suala zima la kujiendeleza kielimu ikiwa ni pamoja na elimu ya sanaa kwa ujumla ili waweze kuandika stori nzuri na kutengeneza mtukio yenye muonekano mzuri.

Filamu alizocheza Fifi ni pamoja na Dar es Salaam, Cross my cine, fake smile, too late, copy, my heart, bongo land part 2, harakati za maisha, trip to America, na nyingine kibao huku kizungumkuti ikiwa amecheza na kuiproduce mwenyewe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents