Bongo Movie

Filamu mpya ya Kanumba kuingia sokoni mwezi huu

Wapenzi wa filamu za marehemu Steven Kanumba watakuwa na uhakika wa kumuona tena staa huyo aliyefariki April mwaka huu kwenye filamu mpya.

Filamu hiyo inaitwa Ndoa Yangu ambapo Kanumba aliigiza na Jackline Wolper.

Ndoa Yangu inatarajiwa kuingia sokoni September 28 ikiwa chini ya usambazaji wa kampuni Steps Entertainment.

Tangu kifo cha Kanumba, hiyo itakuwa ni filamu yake ya kwanza kutoka huku kampuni ya Steps ikidai kuwa imetengenezwa kwa kiwango cha juu na pia haiwezi kukopiwa kirahisi na maharamia kutokana na kutumia teknolojia ya ufungaji filamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents