Burudani

Filamu ya Dr Cheni ‘Nimekubali Kuolewa’ yauza nakala 20,000 ndani ya wiki 1

Msanii wa filamu, Mahsein Awadh maarufu kama Dr Cheni amesema filamu yake ‘Nimekubali Kuolewa’ ndio filamu yake iliyofanya vizuri kuliko filamu zake zote ambapo tayari imeshauza nakala elfu 20,000 ndani ya wiki moja tangu iingie sokoni.

NIMEKUBALI_KUOLEWA_POSTER_PLAIN

Dr Cheni ameiambia Bongo5 kuwa mpaka sasa hajui ni maajabu gani yametokea mpaka filamu hiyo kupendwa kiasi hicho.

“Kwa kawaida ndani ya wiki moja huwaga tunauza nakala elfu 5,000. Lakini kwenye filamu ‘Nimekubali Kuolewa’ imenifungulia njia,” amesema.

“Toka naanza kufanya filamu sijawahi kuuza filamu elfu 20,000 ndani ya wiki moja. Ni dalili nzuri kwangu na inanifanya nione kumbe nilichokifanya ni kitu kikubwa sana. Namshukuru Mungu, waandishi wa habari pamoja na mashabiki wangu,” amesema Cheni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents