Burudani

Filamu ya Jurassic World kuingiza dola bilioni 1 ndani ya wiki mbili tangu itoke

Filamu ya Jurassic World inaendelea kuvunja rekodi za box office duniani.

2972856500000578-0-image-a-30_1435005443077

Jumatatu hii, Universal Pictures ilitangaza kuwa filamu hiyo itavuka mauzo ya dola bilioni 1 kwenye majumba ya sinema duniani ikiwa ni wiki mbili tangu itoke na kuifanya kuwa filamu inayoingiza fedha nyingi kwa haraka katika historia, mtandao wa Comingsoon umeripoti.

Katika wiki yake ya pili pekee filamu hiyo imeingiza dola milioni 106.6 na kufikisha mauzo ya dola milioni 402.8 kwa Marekani peke yake.

Katika siku 11 tu imefikisha mauzo ya dola milioni 500 kwa mauzo katika majumba ya sinema kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents