Uncategorized

Filamu ya maisha ya mwanamuziki kutoka Zanzibar yazoa tuzo kubwa kwenye tamasha la filamu la Golden Globes

Filamu ya Bohemian Rhapsody inayohusu maisha ya muimbaji kinara wa bendi ya Queen ya Uingereza, Freddie Mercury ambaye ni mzaliwa wa visiwani Zanzibar imenyakua tuzo mbili kubwa za tamasha la filamu la Golden Globes.

Brian May and Roger Taylor of Queen with Rami Malek

Brian May (kulia) na Roger Taylor (kushoto) ambao ni waasisi wa beni ya Queen walikuwepo katika tunzo hizo na mwigizaji Rami Malek (katikati)

Lwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo huko Beverley Hills, California nchini Marekani usiku wa kuamkia leo ambapo Bohemian Rhapsody imenyakua tunzo katika kipengele cha filamu bora ya mwaka 2018 na Rami Malek ambaye ndiye alikuwa mhusika mkuu akiigiza kama Mercury amenyakua tunzo ya mwigizaji bora wa kiume.

Filamu nyengine zilizoshinda tunzo ni A Star Is Born ambayo ilipendekezwa sana lakini iliambulia tunzo moja tu. Huku filamu ya Green Book ilikua ni moja kati ya filamu kubwa zilizong’aa baada ya kung’oa tunzo tatu za filamu bora ya kuchekesha, mwigizaji bora msaidizi iliyoenda kwa mwigizaji Mahershala Ali na filamu iliyoandikwa vizuri zaidi.

Mahershala Ali

Ushindi wa Bohemian Rhapsody unakuja kwa kishindo ijapokuwa kulikuwa na vikwazo vingi wakati wa utayarishaji wake.

Muongozaji Mkuu wa awali wa filamu hiyo Bryan Singer alifukuzwa kazi kutokana na kile kilichotajwa kuwa “tabia zisizovumilika” na kuibua taarifa kuwa alikua na mifarakano na Malek wakati wakiandaa filamu. Dexter Fletcher akaletwa ili kumaliza utayarishaji wa filamu hiyo.

Filamu hiyo imevuma sana na kufanya vizuri katika mauzo sokoni na sasa jina la Malek litaingia katika majina pendekezwa ya tunzo maarufu zaidi za Oscar baadae mwezi huu.

Bohemian Rhapsody

Rami Malek (aliye kifua wazi) akimwigiza Freddie Mercury katika filamu ya Bohemian Rhapsody

Katika hotuba yake wakati akipokea tunzo hiyo Jumapili usiku, Malek hakumshukuru Singer, lakini badala yake alitoa heshima kwa bendi ya Queen na kusema kuwa amejawa furaha sana kwa ushindi huo.

“Kwako, Brian May, kwako, Roger Taylor, kwa kuhakikisha kwamba uhalali uhalisia unabaki duniani,” alisema. Wote May na Taylor ambao ni waasisi wa bendi hiyo walihudhuria sherehe hizo.

Alielekeza tunzo hiyo kwa Mercury, ambaye alifariki mwaka 1991, na kuongeza: “Hii na kwaajili yako na kwasababu yako!”H

Mercury ndio alikuwa kiongozi wa band hiyo ya Queen, hivyo filamu hiyo iliakisi zaidi maisha yake.

Kile ambacho wengi hawakifahamu na hakizungumziwi sana katika filamu ni kuwa alizaliwa katika visiwa vya karafuu vya Zanzibar kwenye familia ambayo asili yake ni India na Uajemi. Jina lake alilopewa na wazazi ni Farrokh Bulsara, na baadae akabadili kuwa freddie Mercury.

Mercury alizaliwa katika hospitali ya serikali huko Zanzibar tarehe 5 Septemba mwaka 1946. Wazazi wake Bomi na Jer Bulasara wana mizizi yao huko Uajemi lakini walikuwa pia wameishi nchini India.

Freddie Mercury

Nyumba familia ya Freddie Mercury walikuwa wanaishi Zanzibar

Bomi Bulsara alitokea huko Bulsar Gujarat (ndio maana familia ina jina hilo) na kuhamia Zanzibar kufanya kazi kwenye mahakama kuu kama karani wa serikali ya Uingerezea.

Alimuoa Jer huko India na kumleta Zanzibar. Farrokh mtoto wao kifungua mimba alifuatwa miaka sita baadaye na binti yao, Karishma.

Mercury mara nyingi hakuongeza hadharani kuhusu malezi yake huko Zanzibar.

Farrokh Bulsara

Mwimbaji huyo maarufu alikulia katika mitaa ya Stone town

Waliishi kwenye nyumba nzuri iliyokuwa ikiangalia baharini kwenye mji wa Stone Town ambayo ni sehemu ya kihistoria ya mji wa Zanzibar.

Leo hii mashabiki wake wanaweza kutembea sehemu alizokulia ikiwemo nyumbani kwake na mahakama ambapo baba yake alifanya kazi. Pia kuna mgahawa uitwao Mercury’s.

Miaka ya kwanza ya masomo ya Mercury ni katika shule ya Wamishenari huko Zanzibar ambapo alifunzwa wa watawa wa Kianglikana. Lakini akiwa na umri wa miaka minane wazazi wake waliamua kumpleka shuleni huko India.

Alisomea shule ya St Peter’s Church of England huko Panchgani kusini mashariki mwa mji wa Bombay (sasa Mumbai).

Wakati akiishi na shangazi na mababu zake huko Bombay ndipo akagundua kuwa aliupenda muziki. Pia aliunda bendi yake ya kwanza ya Hectics.F

Freddie alirejea Zanzibar 1963, mwaka ambao visiwa hivyo vilipata uhuru kutoka Uingereza na kumalizia masomo katika shule ya Kikatoliki ya St Joseph’s Convent School.

QUEEN

Freddie Mercury (wapili kushoto) na bendi ya Queen mwanzoni mwa miaka ya sabini

Rafiki yake mmoja kutoka nyakati hizo anakumbuka jinsi walikuwa wakiogelea baharini baada ya kutoka shuleni na pia walivyokuwa wakiendesha baiskeli ufukweni sehemu za kusini.

Lakini nyakati nzuri zilikuwa fupi. Mwaka 1964 mapinduzi yaliwatimua Waarabu waliokuwa wanatawala ambapo yakisiwa watu 17,000 waliuawa. Jamhuri ikaundwa na marais wa Zanzibar na Tanganyika, kwa kusaini mkataba wa umoja. Wakaunda Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Famialia ya Bulsara na wengine wengi wakakimbia visiwa hivyo.

Baadhi ya Washindi wa tunzo za Golden Globes:

  • Filamu bora – Bohemian Rhapsody
  • Filamu bora vichekesho au muziki – Green Book
  • Mwigizaji bora wa kiume – Rami Malek (Bohemian Rhapsody)
  • Mwigizaji bora wa kike – Glenn Close (The Wife)
  • Mwigizaji bora wa filamu/muziki – Christian Bale (Vice)
  • Mwigizaji bora wa kike filamu/muzikil – Olivia Colman (The Favourite)
  • Tamthilia bora – The Americans


Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents