Bongo Movie

Filamu ya ‘Shida za Uani’ yaibuka mshindi wa European Youth Film Competition (EYFC)2017

Filamu fupi ya Animation iitwayo ‘Shida za Uani’, ya kijana Taragwa Anthony ameibuka kidedea kupitia shindano la kuandaa filamu fupi la European Youth Film Competition ililofanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 Septemba 2017 katika Nyumba ya Makumbusho.

Taragwa Anthony mshindi wa shindano hilo

Shindano hili ambalo limechukuwa takriban miezi mitatu liliendeshwa na maudhui ya fursa au changamoto inayosababishwa na ongezeko la idadi ya watu. Hii ilitoa fursa kwa waandaaji wa filamu chipukizi kuonyesha uwezo na umahiri wao wa kuandaa filamu.

Balozi wa Uingereza Roeland Van De Geer, akikabidhi zawadi kwa mshindi

Anthony Taragwa alishinda kupitia filamu yake ya ‘Shida za Uani’ na kufanikiwa kujinyakulia zawadi yenye thamani ya Milioni 7, mshindi wa pili ni Rashid Songoro na Filamu yake ya ‘TONE’ na mshindi wa tatu ni Fred Feruzi na filamu yake ya ‘Bajaji’. Watoto Wangu ya Louis Show ilishinda filamu iliyoshiba maudhui na Watu na Samaki ya Wambura Mwikabe ilishinda filamu iliyopigiwa kura kwa wingi.

Tano bora walipatikana baada ya mchujo kutoka kwa majaji ambao ni Mwl Richard Ndunguru, Issa Mbura, Amil Shvji, Deepesh Shapriya, na Majaji waalikwa Tulanana Buhohela, Dk. Vincensia Shule na Kantarama Gahigiri.

Mashindano haya yaliandaliwa na Umoja wa nchi za Ulaya, Ubalozi wa Uholanzi, Ubalozi wa Ufaransa, the Alliance Française, British Council na Bodi ya Filamu Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents