Bongo Movie

Filamu ya ‘Tatu Chafu’ kuja na mapinduzi ya Bongo Movie (Video)

Wadau wa filamu  na wasanii waliopo nchini wametakiwa kushikamana kwa pamoja katika kutafuta mfumo mzuri utakaowezesha kuwadhibiti wezi wa kazi za wasanii.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mashauri Studio inayofanya kazi ya kuwatambulisha vijana wenye vipaji, Paul Mashauri wakati wa uzinduzi wa filamu mpya ya ‘Tatu Chafu’ inayotarajiwa kuanza kuonyeshwa nchi nzima Desemba 16, mwaka huu.

Mashauri alisema kama wadau watapata mfumo huo basi wataweza kuwadhibiti wezi hao ambao wamekuwa kikwazo kwa wasanii kutofaidi matunda ya ubunifu, jasho na kazi zao.

Alisema takwimu mbalimbali zilizofanya na baadhi ya watu zinaonyesha watanzania wengi wanapenda kuangalia sinema kuliko kitu chochote hivyo ni wakati sasa wa kutafuta mfumo huo ili kuwadhibiti wezi hao na kila msanii anufaike na kazi anayoifanya.

“Sasa hivi filamu ni ajira watu wanaishi, wanakula, wanajenga nyumba hata kusomesha watoto wao kutokana na filamu na takwimu zinaonyesha kwamba watanzania waliowengi wanapenda sana kuangalia sinema hali hii inahamasisha wadau kuweza kuwekeza katika sekta hiyo.

Lakini wadau hawa hawataweza kufanikiwa na kufika malengo waliyojiwekea kama changamoto ya wizi wa kazi za wasanii haitapatiwa ufumbuzi wa kudumu, kinachotakiwa ni kutafuta mfumo madhubuti utawadhibiti kabisa waibaji wa kazi za wasanii wetu,” alisema.

Aidha Mashauri ambaye pia ni mmoja kati ya waanzilishi wa mfumo wa BongohooDz, alisema filamu mpya ya ‘3chafu’ iliyotengenezwa chini ya mfumo huo ni filamu ya kwanza ambayo itazinduliwa na kusambazwa kwa wananchi kupitia mfumo wa matamasha.

“Tutaizindua rasmi fialmu hii Desemba 16 mwaka huu na kuipeleka kwa wananchi kupitia mfumo wa matamasha tutazunguka nchi nzima na katika matamasha hayo tutawapa watu chakula na kufanya vitu mbalimbali vya ubunifu.

Mtu yoyote akipitia mfumo huu wa BongohooDz tutamsaidia kutangaza filamu yake na kumuuzia  hivyo tunawaomba wasanii waje wasisite na kama kuma mtu ana wazo au amekwama kifedha katika kutengeneza filamu aje tutamsaidia,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Mathew Lucas alisema wanawapongeza BongohooDz kwa kazi wanayoifanya ya kuhakikisha filamu zinakuwa na thamani hivyo amewataka wasanii kutumia fursa hiyo kujihimarisha zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents