Burudani

Filamu ya The Avengers’ yafikisha mauzo ya dola bilioni 1.3 duniani kote


Inaonekana The Avengers itavuka matarajio kwa mara nyingine tena.

Filamu hiyo sasa inatishia nafasi ya tatu inayoshikiliwa na filamu ya mwisho ya Harry Potter katika orodha ya filamu zilizoingiza fedha nyingi zaidi.

Harry Potter and the Deathly Hallows, Part 2 imeingiza dola bilioni 1.328 duniani kote na kuwa nyuma ya filamu za James Cameron ambazo ni Titanic inayoshikilia nafasi ya pili na Avatar inayoshikilia nafasi ya kwanza.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, The Avengers sasa imeshaingiza dola bilioni 1.305 duniani kote kwa kuoneshwa kwenye majumba ya sinema.

Inaonesha pia kuwa The Avengers iliyozinduliwa April 11 mwaka huu duniani kote, itaipita The Dark Knight inayoshikilia nafasi ya tatu kwa kuingiza fedha zaidi nyumbani (Marekani).

Kwa sasa The Avengers iliyotayarishwa kwa bajeti ya dola milioni 200, imeshaingiza dola milioni 513.6 kutoka kwenye soko la nyumbani, ambazo ni pungufu ya dola milioni 19.7 tu zilizoingizwa na The Dark Knight nyumbani.

Haijulikani mapato ya The Avengers yatafika kiasi gani lakini makadirio ni dola bilioni 1.4.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents