Filamu Ya We The Party Yazinduliwa Mlimani City

Mwigizaji kijana anayekuja juu Mandela Van Peeble pamoja na Baba Yake Mario Van Peeble ambaye naye pia ni mwigizaji pamoja na mwongozaji usiku wa kuamkia leo wamezindua rasmi filamu yao ya ” We The Party” katika ukumbi wa sinema wa Century Mlimani City jijini Dar-Es-Salaam.

Filamu hiyo ambayo ilitengenezwa Jijini Los Angeles nchini Marekani mwaka huu na kuwashirikisha waigizaji watatu wa familia moja ambapo wawili kati yao ndio wamehudhuria tukio hilo, imeweka historia ya kuwa filamu ya kwanza kuonyeshwa katika ukumbi wa sinema nchini Tanzania kama nchi ya kwanza barani Africa baada ya uzinduzi rasmi wa filamu hiyo nchini Amerika.

Mario na Mandela Van Peebles wapo Tanzania katika mwendelezo wa Tamasha la filamu katika ukanda wa nchi zinazozungukwa na Bahari ya Hindi Tamasha la Filamu la Ziff waliwasili nchini Tanzania kupitia Zanzibar ambapo ni wageni rasmi waalikwa wa ukufunzi wa masuala ya utengenezaji na uigizaji wa filamu katika tamasha hilo la Ziff kwa mwaka huu wa 2012.

Wakihojiwa baada ya kuwasili Mlimani City Mario na Mandela walisema wanayofuraha kubwa sana pamoja na kuona fahari kuzindua filamu hii katika nchi ya Tanzania haswa haswa katika shughuli rasmi ya filamu kwa africa ambayo mwendelezo wake umewafanya kupata nafasi kuionyesha kwa watu ambao hakujua wanamapenzi makubwa na kazi zao.

Aidha tukio hilo la utazamaji wa filamu hiyo ya We The Party kwa mara ya kwanza jijini Dar-Es-Salaam ulitiwa dosari na hitilafu ya spika ambazo zilikuwa hazitoi sauti kwa kiwango kinachostahili kitendo kilichopelekewa Mwongozaji wa filamu hiyo Mario Van Peebles kuamuru uonyeshwaji huo usitishwe hadi hapo spika hizo zitakapofanywa marekebisho.

Akiongea na mwakilishi wa Bongo5 aliyekuwepo katika shughuli hiyo Mario alisema amesikitika kukutana na hali kama hiyo na kuwa spika zilikuwa hazitoi sauti kwa kiwango stahili hasa hasa kwenye vipande ambavyo muziki ulikuwa unahusika na kusema kutosikika vizuri kulikuwa hakumtendei mtoto wake Mandela haki kwani alikuwa anajisikia aibu kwa kudhani inashusha hadhi ya bidhaa yao ambayo ingeonekana kama imetengenezwa kwa kiwango duni.

” Tumekuja hapa toka mbali sana kwa ajili ya kuonyesha filamu hii alafu ghafla mambo hayaendi sawa na kumtia simamnzi mtoto wangu hasa hasa vipande ambavyo vilikuwa na umuhimu kwake kwani yeye ni sehemu ya waigizaji wakuu katika filamu hiyo.

Hata hivyo wahusika wa ZIFF, menejimenti ya ukumbi huo wa sinema na kina Van Peebles wamesema kuwa watalifanyia kazi suala hilo na kesho filamu hiyo itaonyeshwa tena na wageni hao watakuwepo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents