Michezo

Filbert Bayi atimiza miaka 40 tangu avunje rekodi ya mbio za 1500m, lakini asikitika dunia kumsahau…

Jumapili ya February 2, Filbert Bayi ametimiza miaka 40 tangu avunje rekodi ya dunia ya mita 1500, katika mashindano ya jumuiya ya madola.

race1
Filbert Bayi, 1974

Hata hivyo, rekodi hiyo ambayo hadi leo haijawahi kuvunjwa kwenye mashindano hayo imeonekana kusahaulika duniani na hiyo inamuumiza Bayi. Bayi alimaliza mbio hizo kwa dakika 3 na sekunde 32.16, February 2, 1974, huko Christchurch, New Zealand na hadi leo yeye ndio mkimbiaji bora zaidi wa urefu huo kuwahi kutokea duniani.

Filbert-Bayi-3092525

Katika mbio hizo, Bayi alimzidi John Walker aliyekamata nafasi ya pili, nafasi ya tatu ikaenda kwa Ben Jipcho wa Kenya, ya nne kwa Rod Dixon wa New Zealand na ya tano kwa Graham Crouch wa Australia. Bayi, pia alishinda medali ya fedha ya mbio za 3000m za Moscow Olympics mwaka 1980.

“Imesahaulika,” Bayi aliyekuwa nchini Scotland hivi karibuni aliliambia gazeti la Herald Scotland.

“Watu hawasemi kamwe kuhusu Filbert Bayi. Lazima kuna kasoro kwenye hii familia ya riadha sababu watu wengi wametambulishwa kwenye orodha ya wanariadha bora wa muda wote na Shirikisho la Riadha Kimataifa la Riadha, IAAF lakini Filbert Bayi hajawahi kutajwa. Sijui kwanini. Fikiria kuhusu mabadiliko yaliyofanyola kwenye 1500m huko Christchurch. Mbio za 1500m siku zote zilikuwa za taratibu na kisha kuchangamka mwishoni. Lakini mwaka 1974 nilibadilisha hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Na sio watu wengi waliofikiria kuhusu hilo.”

Bayi alisema kidogo kwa sasa watu ndio wameanza kugundua kile kilichotokea.

“Ni miaka 40 sasa na ninahojiwa na watu wa Australia, UK na New Zealand.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents