Tupo Nawe

Firmino amrejesha Philippe Coutinho, Liverpool ‘Nimekumisi sana kaka’

Nyota wa klabu ya Barcelona, Philippe Coutinho amejikuta akirejea Liverpool kwa mara nyingine  tena huku safari hii ikiwa siyo kwaajili ya kuwatumikia majogoo hao wa Anfield.

Phillipe Coutinho made a brief return to Liverpool for the birthday of Roberto Firmino's wife's

Baada ya kuitumikia Liverpool kwa mafanikio makubwa ndani ya miaka mitano, Coutinho alijiunga na miamba hiyo ya Hispania mwezi Januari kwa dau la pauni milioni 145.

Defender Alberto Moreno scrubbed up in a white suit and turtle neck for the event

Usiku wa jana siku ya Jumatano, kiungo huyo mshambuliaji alirejea Merseyside kwaajili ya kumuunga mkono Mbrazili mwenzake Roberto Firmino ambaye alikuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mkewe, Larissa Pereira.

Coutinho was in high spirits as he partied with his former team-mates

Baadhi ya waliyohudhuria kwenye sherehe hiyo ‘all-white affair’ na kunaswa na video ni Firmino na Alberto Moreno ambao wameposti pia kupitia ukurasa wao wa kijamii wa Instagram.

'I've missed you so much brother,' Alberto Moreno captioned a video of him and Coutinho

Coutinho ameonekana akiwa mwenye furaha tele karibu na Firmino, Moreno pamoja na Mbrazili mwenzao Fabinho.

Kupitia Instagram stori, Moreno ameandika ”Nimekumisi sana kaka”, huku wakioneka kufurahi pamoja na Coutinho.

Kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa Larissa Pereira kulikuwa pia na baadhi ya nyota wa klabu ya  Liverpool wanaocheza sasa na hata wa zamani wakionekana wakifurahi kwa pamoja usiku huo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW