Habari

First Lady wa Ufaransa alazwa hospitali kufuatia taarifa kuwa Rais Hollande ana mwanamke mwingine

Mpenzi wa rais François Hollande wa Ufaransa alilazwa hospitali kufuatia kuenea kwa taarifa kuwa kiongozi huyo ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine.

valerie-trierweiler-3
Valérie Trierweiler

Valérie Trierweiler alilazwa hospitali kufanyiwa vipimo na kupumzishwa kutokana na kupokea taarifa hizo Ijumaa iliyopita na kumuumiza moyo. Msemaji wake, Patrice Bianco jana Jumapili alisema kuwa Bi. Trierweiler anatarajia kuruhusiwa kutoka hospitali Jumatatu hii.

Jarida la kila wiki la Ufaransa la Closer Ijumaa iliyopita lilichapisha habari kuhusiana na safari za usiku za rais Hollande kutoka Élysée Palace, ambako yeye na mpenzi wake Ms. Trierweiler wanaishi kwenda nyumbani kwa muigizaji Julie Gayet.

Jarida hilo baadaye liliitoa habari hiyo kwenye website yake kuepuka kushtakiwa ingawa ilisimamia msimamo wake kuwa taarifa hiyo ni ya kweli. Rais Hollande alilaani kitendo hicho cha kuingiliwa maisha yake binafsi ambayo kila raia ana haki nayo.

Rais Hollande ana watoto wanne aliozaa na mgombea urais mwaka 2007, Ségolène Royal.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents