Habari

First Lady wa zamani wa Ivory Coast, Simone Gbagbo aachiwa huru

Mahakama nchini Ivory Coast imemwachia huru first lady wa zamani, Simone Gbagbo, aliyekuwa amefungwa kwa makosa dhidi ya ubinadamu.

Mashtaka yake yalihusiana na vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, pindi mume wake Laurent, alipokataa kushindwa na Alassane Ouattara. Majaji wengi wameyapinga mashtaka kuwa Simone Gbagbo, 67, aliongoza machafuko hayo na alijaribu kununua silaha. Alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 20 kwa kuhatarisha usalama wa nchi.

Ivory Coast imekataa kumpeleka kwenye mahamakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ambako mume wake Laurent Gbagbo anashtakiwa kwa makosa dhidi ya ubinadamu.

ICC imetoa agizo la kukamatwa kwa Simone Gbagbo kwa makosa hayo pia.

Zaidi ya watu 3,000 walipoteza maisha kwenye vurugu za uchaguzi nchini humo mwaka 2010. Laurent na Simone Gbagbo walikamatwa mwaka 2011 baada ya wanajeshi kuvamia kificho walichokuwemo katika mji mkuu, Abidjan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents