BurudaniHabari

Flava za BoNgO + USWISI

Kwa mara ya kwanza ktk historia ya muziki wa kizazi kipya nchini,Wizara ya mambo ya nje ya uswisi wakishirikiana na ChlyKlass Productions pamoja Deiwaka Productions ya hapa Bongo wanakuletea Compilation Cd inayokwenda kwa jina la (Daladala art 05) ikiwa imewashirikisha wasanii wa hiphop kutoka uswisi pamoja na vichwa hatari kutoka Bongo.

CD hiyo ambayo imewashirikisha wasanii kama Mr II a.k.a Sugu,Greis, Fid Q,Baze, Dr Levy, RA,Link,Saigon,A-Bus,Tinga,Nash na David,ina jumla track saba na Intro moja…..ambazo ni Daladala,Welcome to t he Jungle,Mchuma,Oh Meiti,Mikono Juu,Endelezeni na Mdundo mistari.

Songi zote hizo zimerekodiwa na maproducer tofauti tofauti kutoka Uswisi ambao ni Jan Stehle,Link na RA ndani ya Studio mbili tofauti ambazo ni Sofia pamoja na Moskito zote za Dar es salaamni , wakati Mixing na Mastering imefanywa na JaN Stehle ndani ya studio iitwayo (Studio Mama) iliyopo nchini Switzerland.

Waliofanikisha project hiyo nzima wanatajwa kwenye Cd hiyo kuwa ni Wizara ya mambo ya nje ya uswisi,Ubalozi wa Switzerland hapa dar es salaam,Wizara ya Elimu na Utamaduni ya Bongo,BASATA na bila kuwasahau wote walishiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha shughuli hiyo. Tunatumai ushirikiano huu wa aina yake ulioshirikisha mpaka vyombo vikubwa serikalini kama vile wizara za nchi zote mbili…utakuwa ni mwanzo mzuri wa kuusafirisha muziki wetu mpaka kwenye matawi ya juu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents