HabariPicha

Flaviana azidi kuwapagawisha Mexico

Flaviana azidi kuwapagawisha MexicoMISS Universe Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara na kujikusanyia mashabiki lukuki kila sehemu anayopipa nchini Mexico hali inayoonekana kumsafishia njia katika kinyang’anyiro cha dunia cha taji hilo.

Flaviana azidi kuwapagawisha Mexico


MISS Universe Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara na kujikusanyia mashabiki lukuki kila sehemu anayopipa nchini Mexico hali inayoonekana kumsafishia njia katika kinyang’anyiro cha dunia cha taji hilo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinasema kwamba Flaviana amechaguliwa kuwa miongoni mwa warembo 16 watakaoshiriki katika hatua ya nusu fainali sambamba na kushiriki kwenye shindano la kumsaka mrembo mwenye haiba ‘Miss Photogenic’.


Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Lowe Scanad, wadhamini wakuu wa shindano la Miss Universe Tanzania, Nandu Buty, alisema kwamba wamefurahishwa na mafanikio anayoyaonyesha Flaviana.


Miss Universe huyo aling’ara na kuwateka mashabiki, Jumapili iliyopita katika hafla ya kuwapokea warembo wanaoshiriki shindano hilo la dunia, katika tamasha maalumu lililofanyika kwenye kituo cha utamaduni cha Chuapas, Tuxtra Gutierrez.


Flaviana sambamba na warembo wengine, alipata fursa ya kujitambulisha mbele za watu ambao walilipuka kwa kumshangilia mara tu walipomwona. Hafla hiyo iliandaliwa na aliyekuwa Miss Costa Rica ambaye pia ni mcheza sinema maarufu, Maribel Guardia.


Flaviana anatarajiwa kushiriki kwenye fainali za shindano la kumsaka malkia wa Miss Universe 2007, Mexico City Mei 28.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents