Burudani

Flora Mbasha afuta kesi ya talaka dhidi ya mumewe, ‘bado nampenda sana mume wangu’

Ndoa ya Flora Mbasha na mume wake Emmanuel Mbasha bado ipo hai baada ya wawili hao kukubali kuifuta kesi ya talaka iliyodumu kwa takriban mwaka mmoja.

mbasha

Flora ndiye aliyefungua kesi hiyo baada ya kutokea mgogoro kwenye ndoa yao iliyosababishwa na kesi ya kudaiwa kubaka aliyoshtakiwa mumewe. Hata hivyo Emmanuel hivi karibuni alikuwa mtu huru baada ya kushinda.

Mwanasheria wa Flora, Edo November amedai kuwa wawili hao wamekubaliana kuifuta kesi hiyo kwaajili ya uhai wa familia yao yenye watoto wawili.

“Ninachoweza kusema ni kuwa yule ni mume wangu bado ninampenda,” Flora aliiambia AYO TV. “Tunamshukuru Mungu kwa hilo na kila mmoja amekuwa na amani ndani ya moyo wake,” aliongeza.

“Nitaendelea kumpenda siku zote, he is my husband, I love him, I will always love him.” Mbasha alisema bado wana mpango wa kuikuza familia yao. Kuna tatizo moja lakini ili kufanikisha hili – Emmanuel Mbasha hayuko tayari kurudiana na mke wake!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents