Burudani

Floyd Mayweather ajiachia na Paris Hilton

Wakati bondia kutoka nchini Ireland, Conor McGregor’s akiendelea na mazoezi kwa ajili kujiandaa na pambano lake na Floyd Mayweather, Bondia huyo kutoka Marekani ameonekana akijiachia katika jiji la Ufaransa siku ya maonesho ya mavazi.

Mayweather anaeendelea kushikilia rekodi ya kushinda mapambano zaidi ya 40, licha ya kuwa asilimia kubwa ya kushinda pambano hilo anapewa bondia kutokea Ireland. Lakini Mayweather ameonekana akijiamini kwa kujiachia nchini Ufaransa katika jiji la Paris kwenye wiki ya maonesho ya mavazi na mwanadada Paris Hilton.

Mayweather mwenye utajiri zaidi ya dola milioni 105 ameonekana akiwa amevaa koti jeupe katika Philipp Plein Fashion Show siku ya Jumatano katika Cannes akiwa na Hilton, Sofia, Richie na Jeremy Meeks huku tamasha hilo likitazamwa na Eva Longoria.

Pambano kati ya Floyd Mayweather na Conor McGregor linatarajiwa kuwa moja ya pambano gumu na kali sana alisema moja ya bondi mkongwe, Oscar de la Hoya alipokuwa akiongee na kituo cha BBC.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents