Michezo

Floyd Mayweather anatumia zaidi ya $4,000 kumlipa mpishi wake kwa siku

Wakati bondia Floyd Mayweather anajiandaa na mpambano wake na mkali dhidi ya Manny Pacquiao, hutaamini gharama anazotumia kumlipa kwa siku mpishi wake.

928784_810218622393021_2061823877_n

Bondia huyo ambaye jina lake la utani ni ‘Money’, anatumia gharanma sawa na za kununua gari kwa msosi tu kila siku.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Money May humlipa mpishi maarufu na maalumu wa Las Vegas, Chef Q, kiasi cha dola 184,000 kuendeea kumuandalia msosi kila siku mpaka siku ya mpambano May 2.

Chef Q hatozi kiasi hicho kwa mlo ila sababu Floyd mwenyewe ametaka amlipe hivyo hivyo kwakuwa misosi anayopatiwa inastahili kugharamikiwa hivyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents