Michezo

Floyd Mayweather hana kinyongo na utabiri wa Justin Bieber

Ikiwa zimepita siku chache toka msanii wa Pop Justin Bieber atabiri kuwa bondia Conor McGregor, atashinda mpambano unaotarajiwa kufanyika leo hii na kuacha kumtaja swahiba wake Floyd Mayweather kuibuka na ushindi, hatimaye Floyd ameamua kunena ya kwake kuhusu utabiri huo.

Akipiga stori na ‘Hollywood Unlocked’ Floyd ameeelea video ya Justin aliokuwa akihojiwa na TMZ ambapo alitabiri kuwa Conor McGregor ataibuka na ushindi na sio Flody, ndipo bondia huyo wa TMT asema kuwa hana tatizo na msanii huyo wa pop na kila mtu anamaono yake hivyo hawezi kuingilia anachokifanya mtu.

Mpambano wa Floyd Mayweather na Conor McGregor unatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa T-Mobile Arena jijini Las Vegas- Marekani.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents