Habari

Floyd Mayweather Jr aamrishwa kumlipa Manny Pacquiao $113,774

Floyd Mayweather Jr

Bondia Floyd Mayweather Jr. ameamrishwa kumlipa mpinzani wake Manny Pacquiao $113,774 kama adhabu ya kumchafua jina (defamation lawsuit) katika kesi ambayo Pacquiao anasema Floyd alimsingizia mwaka 2009 kuwa anatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Kiasi hicho cha dola 114,000 ni adhabu iliyotolewa na jaji dhidi ya Floyd kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani kama alivyotakiwa kufanya na pia atatakiwa kuwalipa wanasheria wa Pacquiao gharama zote.

Hata hivyo adhabu hiyo haimaanishi kuwa Floyd ameshindwa kesi.

Manny Pacquiao

Mayweather alitakiwa kutokea mahakamani mwezi June-October mwaka jana lakini hakuonekana kwa kisingizio kuwa alikuwa busy akijifua na mazoezi.

Pacquiao alimshambulia kwa kudai kuwa bondia huyo ambaye jina lake la utani ni Money alikuwa akidanganya kuwa yupo busy kwakuwa alipigwa picha akijirusha kwenye klabu za usiku.

Kesi hiyo ina karibu miaka mitatu na bado itaendelea kusikilizwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents