Michezo
Floyd Mayweather kuzichapa na Andre Berto, Septemba 12
Floyd Maywether anatarajia kupanda tena ulingoni September 12 mwaka huu kupambana na Andre Berto.
Floyd atakuwa anajaribu kuifikia rekodi ya bondia Rocky Marciano ya kupigana mapambano 49 bila kupoteza. Berto ameshinda mapambano 30 huku akipoteza mapambano matatu.
Mayweather alisema baada ya pambano lake na Manny Pacquiao kuwa atacheza pambano moja tu la mwisho kabla ya kustaafu masumbwi.