Flyovers in Dar?!

Wakati wowote kuanzia sasa Jiji la Dar es Salaam litaanza kuonekana katika sura mpya kutokana na miradi ya ujenzi wa barabara za juu (fly over) kuwa mbioni kukamilika.


Hayo yalichanwa kweupeee jana bungeni jana na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, wakati akijibu swali la Mbunge wa Magomeni, Muhammed Amour Chomboh, aliyetaka kujua serikali iko tayari kuzishawishi kampuni au mashirika binafsi ya nje na ndani kujenga barabara za juu kama zilivyo nchi nyingine dunia, ili kuondokana na tatizo sugu la foleni.

Waziri Kawambwa, alisema serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) imekamilisha mpango wa barabara za Jiji la Dar es Salaam ambao umebainisha maeneo ambayo yanahitaji kujengwa barabara hizo za juu.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Tazara, Ubungo, Magomeni, Jangwani (Fire), Kamata na makutano ya Barabara ya Nyerere na Kawawa (Chang’ombe.)
Alisema kwa kuanzia, serikali imekubaliana na Japan kujenga barabra za juu katika makutano ya Tazara na Ubungo, ambapo hadi sasa upembuzi yakinifu na usanifu unatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, alisema katika makubaliano hayo, Serikali ya Japan itagharamia ghala za usanifu na ujenzi wakati Serikali ya Tanzania itagharamia fidia ya mali na uhamishaji wa miundombinu ya huduma za jamii kama vile maji na umeme.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents