AwardsBurudaniHabari

FM Academia Wakikausha Kisima Cha Burudani

FM AcademiaMvutano baina ya bendi maarufu jijini za Twanga Pepeta Original na FM Academia umefikia kuleta uhasama unaosababisha upande mmoja kuelemewa na kuonesha kuyumba kutokana na nguvu na jitihada zinazooneshwa na upande mwingine.

FM Academia

 

Mvutano baina ya bendi maarufu jijini za Twanga Pepeta Original na FM Academia umefikia kuleta uhasama unaosababisha upande mmoja kuelemewa na kuonesha kuyumba kutokana na nguvu na jitihada zinazooneshwa na upande mwingine.

 

Wapenzi wa muziki wa Dansi nchini wameonekana kuipa sapoti sana bendi wa FM Academia na kuipa kisogo cha kufa mtu wazee wa kisima cha burudani ambacho hivi sasa kinaonekana kimekauka kutokana na kuyumbishwa na shughuli ya watoto wa kikongo a.k.a wazee wa Ngwasuma ambao wameliteka ile kinoma noma jiji na mikwaju yao ya sebene za hatari

 

Pamoja na kuwa hiki ni kipindi cha mwezi mtukufu ambacho burudani mbali mbali zinaonekana kulegalega lakini kwa Wazee wa Ngwasuma ngoma yao inaendelea kunoga kama kawa utadhani hakuna cha mwezi mtukufu wala nini, ila kizazaa cha kusikitisha kinaendelea kuonekana hasa unapotimba katika kumbi ambazo wanakisima cha burudani hupatikana na kuwakuta wakiimbia viti.
Dah hii inasikitisha lakini ndio mambo ya burudani yalivyo lazima kinara awepo siku zote au sio…. Twanga tokeni upya msikubali kisima cha burudani kikauke…

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents