Tupo Nawe

Forbes wataja mastaa 100 waliongiza mkwanja mrefu zaidi duniani kwa mwaka 2019, Jay-Z, P. Diddy wafunikwa na Kanye West

Jarida la Forbes limetangaza orodha ya majina 20 ya watu maarufu duniani walioingiza mkwanja mrefu kupitia kazi zao wanazozifanya.

Kwenye orodha hiyo namba 1 imechukuliwa na Taylor Swift akiwa ameingiza USD Milioni $185, Kylie Jenner USD Milioni $170 na namba tatu ni Kanye West USD milioni $150.

Kwenye orodha hiyo, Rapper P. Diddy na Jay- Z hawapo kwenye Top 10 badala yake wameshika nafasi ya 28 na 20 kwenye Top 30.

Kwa upande wa michezo, Lionel Messi anayekipiga kunako klabu ya Barcelona ndiye mchezaji wa kwanza duniani, aliyeingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2019 ameingiza USD $127 na kushika namba 4 kwenye orodha hiyo ya Forbes.

Orodha hiyo imeangalia vigezo vya mishahara, Dili za matangazo na biashara wanazofanya mastaa hao. Tazama orodha hiyo kamilia Kwenye hii link – The World’s Highest-Paid Celebrities.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW