Michezo

Franck Ribery nje Kombe la Dunia

Mchezaji wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery amethibishwa na mkufunzi wa timu ya faifa ya Ufaransa kuwa hatashiriki kombe la dunia kutokana na jeraha ya mgongo.
U

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alijeruhiwa mgongoni wakati wa mazoezi siku ya Ijumaa.

“Ilimbidi kuwacha kufanya mazoezi kwa kuwa alikuwa akihisi uchungu mwingi sana,Hataweza kufanya mazoezi wala kucheza kwa majuma kadhaa.” Alisema mkufunzi huyo

Ribery alipelekwa kupigwa picha ya MRI, ambayo ilidhibitisha kiwango cha jeraha hilo.

Riberi alichaguliwa kuwa mchezaji wa tatu bora zaidi duniani mwaka wa 2013 nyuma ya mshindi wa Ballon d’Or Christiano Ronaldo wa Real Madrid na mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents