Picha

Fred Mtoi wa BBC afariki dunia

Fred Mtoi (kulia) alipokuwa akifanya mahojiano na Mheshimiwa Temba (Photo: Jestina George)

Mtangazaji wa BBC Fred Mtoi amefariki dunia usiku mjini London.

Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa mafunzo.

Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.

Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.

Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents