DStv Inogilee!

Fresh 4rom Ireland hadi Bongo!!

Shah SmoothMsanii chipukizi wa kujitegemea Shah Smooth na ambaye anafanyia shughuli zake muziki nchini Ireland,yuko nchini kwa ajili ya kupromote albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Fresh.

Msanii chipukizi wa kujitegemea Shah Smooth na ambaye anafanyia shughuli zake muziki nchini Ireland,yuko nchini kwa ajili ya kupromote albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Fresh.

Shah Smooth
Shah Smooth

Akiteta na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita huku akiwa na copy ya Cd hiyo,Shah ambaye kabla ya kujiingiza kwenye muziki alikua mcheza sarakasi alisema albam hiyo yenye track 8 za kiswahili na moja ya kizungu imefanywa kwenye studio yake mwenyewe iitwayo Riseup Records chini ya Producer wake aliyemtaja kwa jina la Kawele Finger Printer..ambaye alishawahi kuwa mpiga Guitar kwenye Bendi ya (Matimila) ya Dk Remmy Ongala henzi hizooo.

Kwa mujibu wa Shah track zake zimeshaanza kupigwa maredioni tangu wiki iliyopita na hivi sasa anawasiliana na wadosi (Wasambazaji) ili aweze kuitumbukiza albam hiyo sokoni.

Alizitaja track zilizomo kwenye albam hiyo kuwa ni Ingia uwanjani,Fresh,Pesa,Kosa langu silijui,Sukari,Ruka Majoka,Mr Lover,Baba…pamoja na Slicker than your Average (Bonus track).

Kwa sasa kibao chake kinachotamba sana ni (Kosa langu silijui).

 

SOURCE: Darhotwire

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW