BurudaniHabariLady Jay Dee

From Russia wit Luv

Lady Jay DeeMsanii Lady jay Dee ameweka historia kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki na kati kwenda kufanya Show nchini Urusi katika mji wa Moscow, ilikuwa ni kwenye mwaliko maalum ulioandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini humo..

Lady Jay Dee na Captain G mjini MoscowMsanii Lady jay Dee ameweka historia kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki na kati kwenda kufanya Show nchini Urusi katika mji wa Moscow, ilikuwa ni kwenye mwaliko maalum ulioandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa ajili ya watumishi wa serikali na sekta mbali mbali za watu binfasi, utalii, viwanda vidogo vidogo pamoja na wachimbaji wa madini ambao walitakiwa kwenda kuelezea ni namna gani wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza nchini kwetu.

Mkuu wa msafara huo msafara huo alikuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Mheshimiwa Bazil Mramba, wakati mwenyeji wao alikuwa ni balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Patric Chokala, waliweza kufanikisha kile walichokuwa wamekipanga kwani walijitokeza wadau kutoka sehemu mbali mbali duniani ili kujua ni nini kinaendelea nchini Tanzania .

Akiwa ndani ya vazi lililoshonwa kwa kitambaa chenye michoro ya draft ambacho huvaliwa mara nyingi na wamasai, Lady Jay Dee aliweza kuzikonga nyoyo za mataita ambao walikuwepo katika mkutano uliofanyika ndani ya boti ambayo ilikuwa ikiendelea kuzunguka ndani ya mto Moscow .

Kapten Gadner G Habash alikuwa nyuma kumpa Tafu Mamsapu alisema “Mandhari ambayo aliweza kuihisi wakati akiwa ndani ya boti na shughuli ikiendelea anadai ni mithili na ile ya inayoonekana kwenye video ya wimbo wa ‘Step In The Name Of Love’ ya R-Kelly Eh bana ilikuwa si mchezo”

Show ilihudhuriwa na wabongo kibao ambao wako nchini humo kimasomo, walionesha kuufarahia ujio wa msanii Lady Jay Dee kwani ilikuwa ni mara yao ya kwanza kupata burudani kutoka kwa mtanzania mwenzao na Afrika kwa ujumla.

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}


Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents