Michezo

Furaha ya kuifunga Man City, Chamberlain amuanika hadharani mpenzi wake

Kiungo wa klabu ya Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain ameamua kuiweka hadharani picha akiwa na mpenzi wake, Perrie Edwards kupitia mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wao dhidi ya Manchester City.

Alex Oxlade-Chamberlain akiwa na mpenzi wake Perrie Edwards

Kiungo huyu wa Liverpool, Oxlade-Chamberlain alikuwa wakwanza kuipatia bao timu yake wakati ilipocheza na vinara wa ligi Man City na kufanikiwa kuchomo za na ushindi wa mabao 4-3 na kuwafanya vijana wa Guardiola kuchezea kichapo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ligi.

Edwards na Oxlade-Chamberlain mahusiano yao yalianza kuwa wazi kwa miezi 12 sasa

Baada ya kuanza katika mazingira magumu  Anfield, Chamberlain ameanza kuwa kiungo muhimu ndani ya kikosi  cha Jurgen Klopp kufuatiaa kusajiliwa kwa Philippe Coutinho kwenda Barcelona. Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 24 ameshafunga jumla ya mabao matatu .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents