Burudani

Furious 7 yaiwezesha Universal Pictures International kuingiza $1bn kwa mauzo ya tiketi za filamu zake duniani mwaka 2015

Kampuni ya Universal Pictures International imeshaingiza dola bilioni 1 zilizotokana na mauzo ya tiketi za kutazama kazi zake zilizotoka mwaka 2015.

x-2-e1428588090695-1940x1093

Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, kiasi hicho kimetokana zaidi na mauzo ya tiketi ya kuitazama filamu ya Furious 7 iliyoingiza dola milioni 316 nje ya Marekani katika wiki ya kwanza.

Furious 7 inakuwa filamu ya nne kuwahi kuingiza fedha nyingi zake duniani katika wiki yake ya kwanza na kuna uwezekano mkubwa kuwa Fast & Furious 7 ikaingiza hadi dola bilioni 1 hivi karibuni.

Hiyo ni pamoja na ukweli kwamba filamu hiyo tayari imeshapakuliwa kiuharamu mtandaoni kwa zaidi ya mara milioni 2.5 kupitia sites za torrent.

Filamu nyingine ya Fifty Shades of Grey imeisaidia Universal kuiingiza dola milioni 401.2 duniani tangu izinduliwe kwenye Valentine’s Day wakati filamu ya The Theory of Everything ikiwa imeingiza dola milioni 85.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents