Tupo Nawe

Fuse ODG, Diamond Platnumz, N’Golo Kanté wakwara tuzo za BOA Uingereza

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz usiku wa kuamkia leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 ametunukiwa tuzo ya Best Of Africa ya kipengele cha “Philanthropic Endeavour Community Action” inayotokana na mchango wake kwa Jamii .

Wengine walioshinda kwenye Tuzo hizo zilizotolewa Jijini London, Uingereza. Ni Fuse ODG, Wilfried Zaha, Mosamba, N’golo Kanté, Stormyz, Pia tuzo hizo zilihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand.

Tuzo za BOA zinafanyika mwaka huu kwa mwaka wa 8 mfululizo, Na huwa zinawaleta pamoja watu mbalimbali ambao wanaunga mkono na kushiriki kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika bara la Afrika, pamoja na kuwapa Tuzo washindi wa vipengele mbalimbali.

Tuzo za Best of Africa huwa zinawahusisha zaidi wanasoka pamoja na watu mashuhuri ambao wanafanya vizuri kutoka Afrika.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW