Habari

Fuse ODG leo kuichezesha Dar style ya ‘Azonto’

Hitmaker wa Azonto na Antena Nana Richard Abiona aka Fuse ODG leo atawachezesha wakazi wa Dar es Salaam mtindo maarufu wa Azonto atakapotumbuiza kwenye viwanja wa Ustawi wa Jamii.

Show hiyo inatarajiwa kuanza saa 2 kamili usiku kwa kiingilio cha shilingi 10,000 kama ukinunua tiketi mapema na shilingi 15,000 getini.

Jana, Fuse ODG alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye kwenye hoteli ya Kilimanjaro na kuisifia Tanzania kuwa ni nchi inayovutia.

“Lengo langu ni kuuonesha upande mwingine nje ya Africa jinsi ilivyo nzuri, nchi kama Tanzania, ina uoto mzuri wa asili, sio tu Dar es Salaam, Arusha pia ni mji mzuri sana na dunia inapaswa kuona hilo,” alisema.

“Lengo langu napenda nikija kwenye nchi, napenda kuchukua kitu ninachoweza kuionesha dunia, hivyo bila shaka, safari hii ya Dar es Salaam mnaweza kunifundisha kitu na nikirudi niweze kuionesha dunia. Kupitia muziki wangu, naicha dunia ijue kuwa Afrika ni sehemu nzuri kuwepo, hivyo ni heshima kubwa kuwa hapa leo na nasubiria kesho kuungana na watu.”

Katika hatua nyingine, Fuse alipata fursa ya kuongelea interview aliyofanya Chris Brown kwenye kituo cha runinga cha BET miezi kadhaa iliyopita ambapo alisema alijifunza kucheza mtindo wa Azonto nchini Nigeria kupitia Wizkid na kuwafanya wengi waliokuwa wakiangalia show hiyo kuelewa asili ya aina hiyo ya uchezaji ni Nigeria.

“Nadhani ilikuwa kosa ambalo Chris Brown alifanya hata Wizkid amesema yeye mwenyewe nilikuwa naye Ghana miezi michache iliyopita. Azonto ilianzia Ghana, Wizkid kama shabiki wake alitengeneza wimbo kuihusu.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio FM, Rehule Nyaulawa, ambaye kituo chake kimemleta msanii huyo, alisema waliamua kumletea Fuse ODG kwakuwa redio hiyo imejikita kupromote muziki wa Kiafrika na kwakuwa nyimbo za msanii huyo zimekuwa zikiombwa sana kwenye vipindi vyao.

Katika show ya kesho, Fuse atasindikizwa na wasanii mbalimbali wa Tanzania wakiwemo Banana Zorro, H. Baba, Snura, Wakali Dancers, Mapacha aka Magenge ya Mwenge, Dogo Janja, Tunda Man, Madee, Vanessa Mdee, Mabeste, Gosby, Deddy, Menina, Walter Chilambo na Wakazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents