Burudani ya Michezo Live

G Lover alamba tuzo 3, Bob Junior, Dully Sykes, director Eddy na wengene wapewa medali za heshima (Picha)

Mtayarishaji wa muziki, G Lover amepewa tuzo tatu kutoka kwa wadau wa muziki kutoka nchini Uingereza kutokana na mchango mkubwa alioufanya kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Tuzo

Tuzo ya kwanza ni ya heshima kutokana na mchango wake kwenye muziki, na tuzo ya pili ni talented manager kutokana na kusimamia wasanii mbalimbali pamoja na jinsi anavyowasimamia watoto Triple R&Z ambao tayari wamenza kufanya vizuri kupitia project kadhaa walizoziachia. Tuzo ya tatu ni lifetime achievement.

“Mimi nimepewa tuzo 3, Bob Junior, Aloneym  ndio Producers waliofanya hizo kazi na wao wamepata medals za heshima. Pia director wa video Eddy pamoja na Dully Sykes na wao walipata medali.  Aliekuja  kutupa hizi tizo ametoka Uingereza na anaitwa Abdulkareem Mohammed ndio anasimamia kazi za Watoto Triple R&Z kwa Upande wa UK.”

Tuzo hiyo zimetolewa na  Abdulkareem Mohammed ndio anasimamia kazi zao hao Watoto Triple R&Z kwa Upande wa UK.

Bob Junior, Dully Sykes, director Eddy pamoja na producer Aloneym na wao wamekabidhiwa medali za heshima kutokana na mchango wao kwenye project za Triple R&Z.

G Lover pamoja na wadau hao wa muziki
Triple R&Z

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW