G Nako aweka wazi kionjo cha Singeli alichotumia kwenye wimbo ‘Mdundiko’

Msanii wa muziki wa hip hip wa Kundi la Weusi, G Nako amefunguka kuzungumzia kionjo cha muziki wa singeli kilichotumika kwenye wimbo wao wa Mdundiko ambapo pia alikanusha kwamba wameimba muziki wa Singeli.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, G Nako amesema wimbo ‘Mdundiko’ ni aina ya muziki wa trap na sio singeli kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Tunapokea komenti nyingi sana kwenye hili suala hata hapa nilikutana na Sholo Mwamba akawa analizungumzia hilo, lakini ukweli ni kwamba wimbo Mdundiko sio Singeli ila kuna viovjo vidogo vya muziki huo ambavyo tumevitumia, tena nimeimba ‘yeee babaaa poza poza’,” alisema G Nako.

Rapa huyo amesema licha ya komenti hizo ambazo haziwaumizi lakini wimbo huo umepokelewa na mashabiki wengi licha ya kuonekana wamebadilika.

Mapema wiki hii Sholo Mwamba aliiambia Bongo5 kwamba wimbo ni Singeli huku akimshukuru rapa huyo kwa kuonyesha sapoti kwenye muziki huo.

Sikilizi hapa chini video ya wimbo Mdundiko na wewe utoe maoni yako.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW