Burudani

G-Nako: Father Nelly alikuwa bingwa wa kutoa hamasa na kila siku aliichukulia ya ushindi

G-Nako anamkumbuka marehemu Father Nelly kama mtu aliyekuwa ‘positive’, bingwa wa kutoa hamasa na ambaye kila siku aliamini ilikuwa ni ya ushindi.

Akiongea na Bongo5, G-Nako amesema pamoja na kuwa kiungo muhimu wa kundi la Xplastaz, rappers wengi wa Arusha walimchukulia kama kaka yao kimuziki na waliyekuwa wakimsikiliza zaidi.

Rapper huyo wa kundi la Weusi amesema enzi za uhai wa Nelly, alikuwa akikaa naye mara nyingi kusikiliza nasaha zake za msingi katika namna ya kuzikabili changamoto za muziki enzi hizo.

“Alikuwa ni mtu poa, calm, mtu ambaye alikuwa anaona yaani kila siku ni siku ya ushindi,” amesema G-Nako.

“Alikuwa anataka tu Arusha isimame siku zote na bahati mbaya Mungu kamchukua mapema lakini nafikiri ametuinspire kwa kiasi kikubwa, ametupa msukumo mkubwa na ndio maana unaona hadi leo unaona tunafanya hivi.”

Leo ni miaka 11 tangu Father Nelly afariki dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents