Uncategorized

G.Solo awashauri wasanii kuwa wabunifu na wasitegemee muziki pekee

G-Solo

Moja kati ya faida ya makongamano ya kijamii kama Hip Hop Summit ni kupata wasaa wa kukutana na wakongwe na wadau mbali mbali wa muziki huo ambao wapo na wamekuwepo katika nyakati tofauti tofauti za ukuaji wa muziki huo.

Bongo5 imepata wasaa wa kuongea na msanii wa siku nyingi katika game ya Hip Hop na kusema kuwa kwa jitihada zake amefanikiwa kuwatoa Kimuziki baadhi ya wasanii kama vile Nikki wa Pili kwenye track yake ya kwanza ‘’Niaje ni vipi’’, pamoja na kufanya kazi kwenye studio ya Kama Kawa Records.

“Unajua mimi ndiye niliyewatambulisha Marco Chali, na Mbishi Real na wengineo wengi ambao sitawataja, kutokana na muda kuwa mchache, kwa hiyo hata kama nikifa leo, namshukuru mungu nimeacha mchango wangu wa dhati katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya”. Hayo ndiyo yalikuwa maneno yake ya utangulizi katika maongezi yetu,”alisema G.

G Solo anasema, kwa sasa, baada ya kuimba sana, amaeamua kubadilika kidogo na kuzikita harakati zake za kuelimisha jamii kwa kutumia uandishi. “Mpaka sasa nimefanikiwa kutoa kitabu kimoja ambacho kinaitwa ‘’Harakati za Bongo Flava na Mapinduzi,”alisema.

“Kitabu kinazungumzia nyakati na harakati zake mbali mbali za ki muziki toka miaka ya tisini hadi sasa, ambazo zimepitia wilaya, tarafa, kata na mikoa tofauti tofauti ya Tanzania.

“Nimeamua kubadilisha upepo kidogo ili niweze kuonyesha uwezo wangu wa kuwakilisha, siyo kwa kuimba tu, bali hata uandishi naweza, na nina kitabu kingine, ambacho kitaitwa ‘’Gereza huru’’ kwa mimi sijibani kimawazo ninaweza nikafanya mambo mengi sana.”

“Wasanii tunahitaji kujaribu kujiongeza kila tunapopata nafasi, kwa sasa nategemea kutoa filamu yangu ambayo nimechagua kuipa jina la ‘’kizazi cha Laana’’, anaendelea na kusema kitu ambacho kimemsukuma kufikiria kufanya filamu hiyo ni hali halisi ya kimaisha ambayo amepambana nayo katika maisha yake.

“Nilikaa chini na kufanyia uchunguzi mambo mbali mbali yaliyonikuta na kagundua siko peke yangu, jamii nzima inakumbwa na matatizo kama yaliYonikuta, basi nikaamua kufanya filamu ambayo itawakilisha mawazo yangu ili iwe chachu ya mabadiliko kwa wengine”.

Aidha aliwashauri wasanii wasitegemee Muziki tu, na kwamba, wajipambanue kwa njia tofauti tofauti za kisanaa, kiakili, kiubunifu kama yeye ambavyo alivyojaribu kufanya. “Fuatilieni mfano wangu, nimeandika kitabu na sasa nipo njiani kutoa filamu yangu, hii ni dhahiri kwamba nimejaribu kutotaka kutegemea Muziki tu.”

Alimalizia kwa kusema litakuwa jambo zuri kwa wasanii wakongwe kuwasaidia wasanii wachanga kuona nuru na mwanga na kuendeleza harakati ambazo zitasaidia jamii kuelekea kwenye mabadiliko chanya ya kijamii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents