G-Unit Kushuka Afrika Kusini

G-Unit Kushuka Afrika Kusini. Onesho hilo linatarajiwa kuwashirikisha wakali wa kundi hilo likiongozwa na 50 Cent, Young Buck, Lloyd Banks na Tony Yayo wote kwa pamoja wakiunda kundi lililojizolea marundo ya sifa la G-Unit.

G Unit


 


Onesho hilo linatarajiwa kuwashirikisha wakali wa kundi hilo likiongozwa na 50 Cent, Young Buck, Lloyd Banks na Tony Yayo wote kwa pamoja wakiunda kundi lililojizolea marundo ya sifa la G-Unit.


 


Wakali hao wanatarajiwa kupiga show yao ya kwanza siku ya tarehe 1 Mei jijini Johannesburg kabla ya kwenda kwa ajili ya kupiga show katika ukumbi wa Beliville Vellodrome siku ya Jumamo ya tarehe 3 mwezi Mei.


 


Onesho hilo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Virgin Mobile ikishirikiana na SABC1 “tunajivunia sana kwa kumudu kumleta msanii 50 Cent hapa Afrika kusini kwani muziki upo katika kile ambacho tunakifanya kutokana na mapenzi ya wateja wetu na ndio maana tunaweka pesa yetu pale penye wapenzi wengi” alisema CEO wa kampuni ya Virgin Mobile.


 


Mpaka sasa Tiketi zimeshaanza kuuzwa nchini humo tayari ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wakali hao ambao watatua na kufanya makamuzi pande zile.


 


Je Bongo lini!? Au Mei hiyo hiyo……

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents